MAREKANI-TRUMP-BIDEN-SIASA

Uchaguzi wa urais wa Marekani: Trump na Biden wavutana katika mdahalo wa mwisho

Siku 12 kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, rais anaye maliza muda wake Donald Trump na mshindani wake mkuu katika uchaguzi huo Joe Biden walishambuliana tena katika mdahalo wa mwiho lakini kwa kwa njia nzuri kuliko wakati wa mdahalo wao wa kwanza.

Rais wa Marekani Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden wakati wa mdahalo wao wa pili na mwisho huko Nashville, Oktoba 22, 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden wakati wa mdahalo wao wa pili na mwisho huko Nashville, Oktoba 22, 2020. Chip Somodevilla/Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi jioni, Donald Trump alianza mdahalo huo kwa sauti ya utulivu, na mazungumzo, ingawa yalikuwa ya kusisimua, yalionekana ni yenye utulivu ikilinganishwa na mdahalo uliotangulia.

Mdahalo wa pili na wa mwisho wa kampeni za kugombea urais ulifanyika katika mji wa Nashville katika jimbo la kusini la Tennessse.

Katika mdahalo huo waligusia masuala nyeti kama janga la COVID-19, maswala ya ubaguzi wa rangi, mabadiliko hali ya hewa na sera ya kigeni.

Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden amemshtumu rais Donald Trump, akisema hana mkakati wowote juu ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

amebaini kwamba Trump hafai tena kuwa rais wa nchi hiyo kutokana na vifo vya wamarekani zaidi ya laki mbili viliyvosabaishwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Hata hivyo rais Trump alijitetea akisema chanjo dhidi ya virusi vya corona inakaribia kupatikana nchini Marekani.

Wakati huo huo Biden alimtaka Trump aonyeshe marejesho yake ya kodi badala ya kuwapakazia wenzake maneno yasiyo na ushahidi.

Trump alijibu kuwa ataweka bayana haraka iwezekanavyo, na kwamba alilipa kodi mapema kabla ya wakati katika miaka kadhaa iliyopita, amesema alilipa mamilioni ya dola.

Kura za maoni zinaonyesha Biden anaongoza dhidi ya Trump, ingawa mashindano ni makali katika baadhi ya majimbo yanayogombewa ambayo yana nafasi kubwa ya kubadili mambo uchaguzi huo wa urais nchini Marekani.