COLOMBIA-USALAMA-SIASA

Colombia: Afisa mwandamizi wa ELN auawa Choco

Rais wa Colombia Ivan Duque.
Rais wa Colombia Ivan Duque. Présidence colombienne

Vikosi vya usalama vya Colombia vimemua kamanda wa waasi wa Jeshi la Kitaifa la Ukombozi (ELN) wakati wa operesheni katika mkoa wa pwani wa Choco, rais Ivan Duque amesema katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni Jumapili jioni.

Matangazo ya kibiashara

Kamanda aliyejulikana kwa jina la siri la "Uriel", maarufu kwa kuonekana kwenye vyombo vya habari na video za mkondoni, alilihusika katika visa mbalimbali vya utekaji nyara na mauaji ya wanaharakati na maafisa wa vikosi vya usalama, na kwa kuwaangiza kwa nguvu katika kundi lake watoto, amesema rais wa Colombia akimbatana na wawakilishi wa polisi na jeshi.

Kundi la ELN linaloundwa na wapiganaji 2,000, mwezi Januari 2019 lilifanya shambulio la bomu lililotegwa katika gari dhidi ya chuo cha polisi huko Bogota, shambulio lililogharimu maisha ya watiu 22 na kuvunja uwezekano wa kufungua mazungumzo na serikali ya Duque, iliyokuwa ipinga kuketi kwenye meza ya mazungumzo na waasi hao kabla hawajawaachia mateka wao wote walio kuwa mikononi mwao.