MAREKANI-HAKI

Baraza la Seneti la Marekani lamuidhinisha Jaji Amy Coney Barrett katika Mahakama Kuu

Rais Donald Trump mwenyewe ndiye alimteua wakili wa kihafidhina kuchukua nafasi ya Dean Ruth Bader Ginsburg, ambaye alifariki dunia mnamo Septemba 18.

aji wa kihafidhina Amy Coney Barrett katika Ikulu ya White House, Septemba 26, 2020.
aji wa kihafidhina Amy Coney Barrett katika Ikulu ya White House, Septemba 26, 2020. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Kuidhinishwa kwake, ambao sio mshangao, unakuja wakati unaofaa wakati kampeni ya uchaguzi inaingia katika siku za lala salama kabla ya Uchaguzi wa urais uliopangwa Novemba 3.

Hayo yanajiri wakati rais anayemaliza muda wake, Donald Trump, licha ya kupata kura ndogo kulingana na uchunguzi, anajaribu kuhamasisha wapiga kura wake.

Wakati huo huo Amy Coney Barrett ameapishwa kuwa jaji wa mahakama ya juu Marekani baada ya kupigiwa kura na baraza la Seneti lililogawika pakubwa, ambapo Warepublican waliwazidi nguvu Wademocrat na kumuidhinisha.

Chaguo la Trump kujaza nafasi iliyoachwa kufuatia kifo cha aliyekuwa jaji wa kiliberali marehemu Ruth Bader Ginsburg kimsingi linafungua enzi mpya ya maamuzi kuhusu utoaji mimba, ulinzi wa huduma za afya na hata kuchaguliwa kwa Trump mwenyewe. Wademocrat walishindwa kuzuia matekeo hayo, ambayo ni jaji wa tatu kuchaguliwa na Trump kwenye mahakama hiyo, wakati Warepublican wakiendelea na harakati za kuifanyia mageuzi idara ya mahakama.