Pata taarifa kuu
BOLIVIA-MORALES-HAKI

Ivo Morales kurejea Bolivia

Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Buenos Aire, Argentina, Februari 21, 2020.
Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Buenos Aire, Argentina, Februari 21, 2020. RONALDO SCHEMIDT/AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Jaji mmoja nchini Bolivia amefuta waranti wa kukamatwa uliyotolewa dhidi ya Evo Morales, ikimruhusu kurudi Bolivia bila kuwa na wasiwasi wa kukamatwa.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Desemba mwaka jana, mwendesha mashtaka wa umma wa Bolivia alitoa waranti wa kukamatwa dhidi ya rais huyo wa zamani kwa madai ya uasi na ugaidi.

Chama cha Kisoshalisti cha Evo Morales kimerejea mamlakani nchini Bolivia, baada ya mgombea wake, Luis Arce, kushinda kwa 55.10% ya kura.

Evo Morales bado ni kiongozi wa chama cha Movement for Socialism (MAS), chama cha Luis Arce, lakini Bw. Arce alitangaza kwamba Evo Morales hana "jukumu lolote" katika serikali yake.

Evo Morales hajasema ikiwa atarudi Bolivia au kutoa tarehe ya kurudi kwake nchini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.