MEXICO-USALAMA

Maiti 59 zagunduliwa katika kaburi la halaiki Mexico

Miili hamsini na tisa imepatikana katika kaburi la halaiki lililogunduliwa katikati mwa Mexico, mamlaka imesema. Kaburi hilo liligunduliwa katika mji wa Salvatierra katika jimbo la Guanajuato, eneo la kivita kati ya makundi hasimu ya wafanyabiashara haramu.

Makaburi ya pamoja yaemendelea kugunduliwa nchini Mexico.
Makaburi ya pamoja yaemendelea kugunduliwa nchini Mexico. PEDRO PARDO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Angalau miili kumi ilikuwa ya wanawake na miili mingi ilikuwa ya vijana, kulingana na taarifa za Karla Quintana, mkuu wa Tume ya Kitaifa ya Utafiti nchini Mexico.

Uhamasishaji wa familia za watu waliopotea uliwezesha ugunduzi mkubwa wa makaburi ya siri huko Guanajuato, Karla Quintana aliambia mkutano na waandishi wa habari Jumatano alasiri.

Jimbo la Guanajuato lilirekodi visa 2,250 vya mauaji kati ya mwezi Januari na Agosti mwaka huu, kulingana na takwimu rasmi, ongezeko la zaidi ya 25% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.