BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini Brazil yapindukia zaidi ya 160,000

Brazil imerekodi visa 10,100 vilivyothibitishwa vinavyotokana na virusi vya Corona baada ya vifo vipya 190 kuthibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imebaini.

COVID-19 imeua watu wengi Brazil.
COVID-19 imeua watu wengi Brazil. REUTERS/Bruno Kelly
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya milioni 5.5 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Brazil na vifo 160,074 vimethibitishwa, kulingana na takwimu za serikali.

Kwa upande mwingine Mkuu wa shirika la Afya duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema anajiweka karantini baada ya kukutana na mtu ambaye sasa amebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Tedros ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema bado yuko na afya njema bila dalili za COVID-19, lakini atasalia karantini kwa siku kadhaa zinazokuja kama taratibu za WHO zinavyoelekeza.

Hayo yanajiri wakati nchi nyingi za Ulaya zinakambulmiwa na wimpi jipya la mlipuko wa COVID-19. Baadhi ya nchi za bara hilo zimechukuwa makata mapya ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo hatari.

Maambukizi ya virusi vya Corona hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 279,000 barani Ulaya tangu vilipozuka nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.