MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Kati ya Trump na Biden, nani atashinda uchaguzi wa urais

Kampeni zimeingia katika dakika za lala salama nchini Marekani kuelekea siku ya upigaji kura Jumanne wiki hii Novemba 3. Uchaguzi ambao kila mmoja anasubiri kujuwa nanai kati ya Donald Trump na Joe Biden ataibuka mlshindi.

Joe Biden na Donald Trump.
Joe Biden na Donald Trump. AP/Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amefanya kampeni za mwisho katika majimbo matano yanayowaniwaa, na ameendelea kuwaambia wafuasi wake kuwa mpinzani wake Joe Biden hafai kuwa rais wa nchi hiyo.

“Mpango wa Biden na Harris kuhusu nishati sio mzuri kwa ajali ya maisha yetu, bila shaka mpango wake utasabisha bei kuongezeka na ataongeza kodi yenu katika majimbo yenu, mnamfahamu na ninamfahamu, sio mtu mwema, “ amesema Donald Trump akiwaambia wafuasi wake katika majimbo ya Iowa na Michigan.

Biden naye amekuwa katika jimbo la Pennsylvania na amewaambia wafuasi wake kuwa lazima wajitokeze kwa wingi ili kuondoa utawala wa Donald Trump, ambaye amitumbukiza Marekani katika matatizo mbalimbali, hasa baada ya kushindwa kusimamia ugonjwa hatari wa COVID-19.

“Hii ni mara ya mwisho kwa Trump kuwania, alishinda jimbo hili kwa kura zaidi ya Elfu 44, kwa hivyo kila kura ni muhmu, uamuzi wa kubadilisha taifa hili upo mikononi mwenu, hakuna anachoweza kufanya kuzuia watu kupiga kura, hata afanye nini, ” amesema Joe Biden.

Mnamo mwaka 2016, dhidi ya Hillary Clinton, Donald Trump alipata ushindi wa kura nyingi katika majimbo ya Pennsylvania, Wisconsin na Michigan, majimbo matatu ambayo yalikuwa yakipigia kura chama cha Democratic kwa miongo kadhaa.

Tayari wapiga kura Milioni 90 wameshapiga kura za mapema kupitia njia ya posta.