MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Edison Research: Biden aongoza kwa kura 205 za wajumbe maalumu dhidi ya 171 za Trump

Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, Septemba 15, 2020.
Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, Septemba 15, 2020. AP Photo/Patrick Semansky

Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden anaongoza kwa kura 205 za wajumbe maalumu dhidi ya 171 ambazo amepata rais kutoka chama cha Republican Donald Trump, kulingana na makadirio ya shirika la Edison Research.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika hilo jumla ya kura 376 kutoka kwa wajumbe maalumu zimepigwa.

Jumla ya wajumbe maalumu 538 wanaunda bodi ya Uchaguzi. Ili kuibuka mshindi mgombea anapaswa kupata kura zisizopungua 270 za wajumbe maalumu, Kila jimbo maalumu lina idadi ya kura kulingana na idadi yake ya watu na kwa jumla ziko kura 538.

Wamarekani zaidi ya milioni Mia moja wamepiga kura ya kuamua iwapo watamrudisha madarakani Donald Trump au wataamua kuleta mabadiliko kwa kumchagua mgombea wa chama cha Demokratik Joe Biden, baada ya wanasiasa hao wawili kupambana vikali kwenye kampeni zao katika muktadha wa janga la maambukizi ya virusi vya Corona.

Mpaka sasa wamarekani zaidi ya laki 2 na 33 alfu wameshakufa kutokana na maambukizi ya virusi hivyo na wengine wanaokaribia milioni 10 wameambukizwa huku maambukizi yakiongezeka kila siku.