MAREKANI-TABIA NCHI

Marekani yajitoa rasmi kwenye mkataba wa hali hewa wa Paris

Marekani imetangaza kwamba inajiondoa rasmi kwenye mkataba wa hali ya hewa uliofikiwa jijini Paris, nchini Ufaransa, ikitimiza ahadi ya muda mrefu iliyotolewa na rais Donald Trump.

Donald Trump alitangaza kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Juni 2017 nia yake ya kujitoa kwenye mkataba huo, akilaani athari kubwa kwenye uchumi wa Marekani.
Donald Trump alitangaza kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Juni 2017 nia yake ya kujitoa kwenye mkataba huo, akilaani athari kubwa kwenye uchumi wa Marekani. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo unakuja wakati wananchi wa Marekani walipiga kura Jumanne wiki hii kumchagua rais wao kati ya Donald Trump wa chama cha Republican na Joe Biden wa chama cha Democratic.

Matokeo ya kura ndio yataamua ikiwa uamuzi huo wa ni wa moja kwa moja. Mpinzani wa Donald Trump, Joe Biden, ameahidi kwamba Marekani itajiunga upya na mkataba huo atachukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Donald Trump alitangaza kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Juni 2017 nia yake ya kujitoa kwenye mkataba huo, akilaani athari kubwa kwenye uchumi wa Marekani. hata hivyo, rais Trump hajafanikisha nia yake hadi sasa, masharti ya mkataba huo yamemzuia kufanya hivyo.

Marekani ni moja tu ya nchi 197 zilizosaini mkataba huo ambayo imejiondoa kwenye mkataba uliyotiwa saini mwaka 2015 katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.