UCHAGUZI MAREKANI 2020

Mbali na vita ya urais, Democrats na Republicans, wanachuana katika seneti

Wakati huu macho na masikio yakiwa ni katika matokeo ya kiti cha urais, Democtrats na Republicans, wanachuana pia katika mbio za kuwa na udhibiti wa bunge la Congress na Seneti.

Watu wakitazama usiku wa uchaguzi kwenye televiseni kubwa iliyowekwa ukutani karibu na ikulu ya White House huko Washington, Novemba 3, 2020.
Watu wakitazama usiku wa uchaguzi kwenye televiseni kubwa iliyowekwa ukutani karibu na ikulu ya White House huko Washington, Novemba 3, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mbio za seneti, gavana wa zamani wa Democrats, John Hickenlooper, amefanikiwa kumuangusha mgombea wa Republicans, Cory Gardner.

Kiongozi wa wengi katika seneti kupitia Republicans, Mitch McConnell pamoja na mshirika wa karibu wa rais Trump, Lindsey Graham, wote wawili wamefanikiwa kutetea viti vyao.

Katika mji wa Alabama, mgombea wa Republicans Tommy Tuberville, amefanikiwa kushinda kiti kilichokuwa kinakaliwa na mgombea wa Democrats, Doug Jones.

Nchini Marekani, Seneta uhudumu kwa muda wa miaka 6, na kila baada ya miaka miwili karibu robo tatu ya viti katika seneti hugombaniwa.

Kwa mwaka huu zaidi ya viti 35 kati ya 100 vinawaniwa, na ili chama kipate uongozi katika bunge hilo vinahitaji viti 51.

Katika bunge na seneti itakayoongozwa na Democrats, watakuwa na uwezo wa kuzuia mipango mingi ya rais Trump ikiwa atashinda kwa muhula wa pili au kupitisha ajenda za Joe Biden ikiwa atachaguliwa kuwa rais.