MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Trump adai ushindi wakati zoezi la uhesabiji kura halijakamilika

Rais anaye maliza muda wake Donald Trump ametangaza usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano kwamba matokeo ya uchaguzi yalikuwa "ya kushangaza" na kudai ushindi dhidi ya Joe Biden wakati matokeo katika majimbo kadhaa muhimu bado hayajaamuliwa.

Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa kampeni yake i huko Roma, Georgia, Novemba 1, 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa kampeni yake i huko Roma, Georgia, Novemba 1, 2020. AP Photo/Brynn Anderson
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kweli, tumeshinda uchaguzi huu," amesema katika hotuba kutoka Ikulu ya White Haouse, na kuongeza kuwa "kundi dogo la watu" walikuwa wakijaribu kumuibia ushindi.

Rais anayemaliza muda wake kutoka chama cha Republican amedai ushindi katika majimbo ya Florida, Ohio, Texas lakini pia Georgia, North Carolina na kusema anaelekea kuapata ushindi katika jimbo la Pennsylvania "kwa kiwango kikubwa".

Hakuna matokeo ya uchaguzi, hata hivyo, yanathibitisha kufikia sasa kuwa Trump anaongoza kwa jumla ya majimbo dhidi ya Joe Biden.

Shirika la Edison Research linaonyesha kuwa Trump hana uhakika katika hatua hii ya kushinda kwa kura 270 zinazohitajika kwa uchaguzi wake kwa muhula mwingine.