MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi Marekani 2020: Trump na Biden wapelekana puta

Wananchi wa Marekani wamepiga kura kumchagua rais wao katika uchaguzi ambao wengi wanataraji mabadiliko makubwa. Zaidi ya watu milioni 100 walikwisha piga kura zao za mapema.

Joe Biden na Donald Trump.
Joe Biden na Donald Trump. Studio Graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Tayari uchaguzi huo ambao wagombea wote wawili kutoka chama cha Republican Donald Trump na makamo wa zamani wa rais Joe Biden kutoka chama cha Democratic wanaendelea kuonyesha nguvu zao kwa wafuasi kutoka majimbo mbalimbali nchini Marekani.

Wamarekani zaidi ya milioni Mia moja wamepiga kura ya kuamua iwapo watamrudisha madarakani Donald Trump au wataamua kuleta mabadiliko kwa kumchagua mgombea wa chama cha DemokratiC Joe Biden, baada ya wanasiasa hao wawili kupambana vikali kwenye kampeni zao katika muktadha wa janga la  maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa uchaguzi huo umeliligawanya taifa hilo kwa kiwango kisichokuwa cha kawaida kutkana na mitazamo mbalimbali.

Kulingana na matokeo ya awali mchuano kati ya wawili hao ni mkali katika majimbo kadhaa.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Biden ameshinda kwenye majimbo ya Virginia, Delaware,Vermont Connecticut, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Rhode Island huku Trump akiyanyakua majimbo la Virginia magharibi, Kentucky, na South Carolina, Alabama, Mississippi, Oklahoma na Tennessee.

Mpaka sasa Joe Biden anaongoza kwa kura za wajumbe maalum 131 na Trump akiwa na idadi ya kura 98 za wajumbe maalum. Matokeo yanaendelea kutangazwa.

Katika Jimbo la Florida rais anaye maliza muda wake Donald Trump anaongoza kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.

Trump anaelekea kupata faida kwa wapiga kura wenye miaka 65 na zaidi kwa (51% kwa 48%).

Kura ya maoni imempa ushindi Biden, lakini matokeo ya awali yameonesha kuwa mchuano ni mkali hasa katika majimbo yanatarajiwa kuamua matokeo kati ya wawili hao.