MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Wajumbe maalumu wana shinikizo gani kwa uchaguzi Marekani

Licha ya Wamarekani kupiga kura, rais wa nchi hiyo huchaguliwa na kundi la wajumbe 538 ambao huamua mshindi. Ni kwanini hali huwa hivyo na inamaanisha nini ?

Kwenye lango la kituo cha kupigia kura huko Houston, Texas, Novemba 3, 2020.
Kwenye lango la kituo cha kupigia kura huko Houston, Texas, Novemba 3, 2020. REUTERS/Go Nakamura
Matangazo ya kibiashara

Mfumo wa Uchaguzi wa Marekani kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, umewapa mamlaka wajumbe hao kumchagua mshindi.

Waliaondika Katiba ya Marekani waliamua kuwe na wajukbe hawa kwa hofu kuwa huenda, wapiga ikura wasifanye maamuzi sahihi lakini pia ilihpfiwa kuwa majimbo yenye iudadi kubwa ya watu wangekuwa na nafasi kubwa ya kuamua mshindi wa Uchaguzi nchini humo.

Kila jimbo nchini Marekani angalau lina wajumbe watatu, lakini jimbo la Califonia ambalo ndilo lenye watu wengi nchini Marekani lina wajumbe 55, huku Texas likiwa na wajumbe 38.

Ili kuibuka mshindi, mgombea anastahili kupata angalau kura 270 za wajumbe hao.

Mwaka 2016, Hillary Clinton alishinda Uchaguzi wa wapiga kura lakini, Trump akamshinda katika kura za wajumbe.

Mfumo huu pia unatarajiwa kuamua mshindi katika Uchaguzi huu.