MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Wamarekani waendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais

Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameingia katika hatua muhimu, huku rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wakiwa na ushindani mkali katika majimbo muhimu.

Wakati hesabu za kura bado zinaendelea huko Marekani, bado kuna majimbo kadhaa au zaidi ambayo matokeo yake bado hayajulikani ikiwa ni pamoja na "majimbo" kadhaa muhimu, ambayo yanaweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi uchaguzi wa rais.
Wakati hesabu za kura bado zinaendelea huko Marekani, bado kuna majimbo kadhaa au zaidi ambayo matokeo yake bado hayajulikani ikiwa ni pamoja na "majimbo" kadhaa muhimu, ambayo yanaweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi uchaguzi wa rais. REUTERS/Carlos Barria/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Huku kukiwa na ushindani mkali , matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo huenda yasijulikane kwa siku kadhaa.

Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Donald Trump amehoji tena mchakato wa uchaguzi wa urais unavyoendelea, akizitaja "kura za kushangaza" zilizochanganywa na kura zake katika baadhi ya majimbo.

"Jana usiku nilikuwa nikiongoza kwa kura nyingi katika majimbo mengi muhimu, ambayo karibu yote yanayoongozwa na kudhibitiwa na chjama cha Democratic. Halafu, moja kwa moja, walianza kupoteza kura zangu kwa njia isiyoeleweka kwani kura za mshangao zilikuwa zimehesabiwa. Kwa kweli waliniibia kura, " amesema Donald Trump.

Kulingana na msimamizi wa kampeni ya Joe Biden, mgombea huyo kutoka chama cha Democratic anaelekea kushinda uchaguzi na anatarajia kupata wajumbe maalumu 270 wanaohitajika.

Wakati huo huo Donald Trump amesema atapinga matokeo ya uchaguzi mahakamani bila kutoa ushahidi wa kufanyika kwa udanganyifu.