BRAZILI-HAKI

Brazil: mtoto wa Jair Bolsonaro atuhumiwa makosa ya ufisadi siku kumi kabla ya uchaguzi

Flávio Bolsonaro, seneta na mtoto wa kwanza wa rais wa Brazil Jair Bolsonaro, ameshtakiwa rasmi kwa ufisadi katika kesi ya kuanzia mwaka 2003 hadi 2018. Hapa Brasilia, Aprili 24, 2020.
Flávio Bolsonaro, seneta na mtoto wa kwanza wa rais wa Brazil Jair Bolsonaro, ameshtakiwa rasmi kwa ufisadi katika kesi ya kuanzia mwaka 2003 hadi 2018. Hapa Brasilia, Aprili 24, 2020. REUTERS/Ueslei Marcelino

Nchini Brazil, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Rio de Janeiro imepokea mashtaka ya ufisadi dhidi ya Seneta Flavio Bolsonaro, mmoja wa watoto wa rais Jair Bolsonaro.

Matangazo ya kibiashara

Flavio Bolsonaro anashutumiwa hasa makosa ya ubadhirifu wa pesa za umma na utakatishaji wa pesa haramu. Hi ni kesi ya kwanza kwa mmoja katika familia ya Bolsonaro tangu Jair Bolsonaro aingie madarakani.

Hii ni taarifa mbaya wa kiongozi wa mrengo wa kulia, siku chache kabla ya uchaguzi wa serikali ya mitaa.

Ni baada ya kuanzisha mfumo ambao Wabrazil wanauita kama "Rachadinha" ambapo Flávio Bolsonaro anakabiliwa na hatari ya kushtakiwa.

Flavio Bolsonaro, mtoto wa kwanza wa rais na seneta anatuhumiwa na waendesha mashtaka wa Rio de Janeiro kwa kushirikiana na kundi la uhalifu na utumiaji mbaya wa pesa za umma wakati alikuwa mbunge wa jimbo la Rio kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2018.

Hata hivyo, Kwenye mitandao ya kijamii, Flávio Bolsonaro ametangaza kwa mara nyingine kuwa hana hatia wakati ombi la upande wa mashtaka sasa litachunguzwa na jaji, ambaye atalazimika kuamua ikiwa mtoto wa rais atakabiliwa na mashitaka au la.

Uamuzi huu utatolewa kabla tu ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Brazil: duru ya kwanza itafanyika ndani ya muda wa siku 10, mnamo Novemba 15. Uchaguzi huu unaonekana kama kipimo kwa umaarufu kwa Jair Bolsonaro, anayekosolewa sana kwa jinsi anavyoshughulikia janga la Corona, ambalo tayari limeua zaidi ya Wabrazil 160,000.