Covid-19: Visa vipya 100,000 vyathibitishwa Marekani
Karibu visa vipya 100,000 vya maambukizi ya ugonjwa hatari wa COVID-19 vimeripotiwa nchini Marekani katika muda usiozidi saa ishirini na nne.
Imechapishwa:
Hii ni rekodi mpya siku moja baada ya uchaguzi wa urais, kulingana na takwimu za kituo kinachozuia na kudhibiti magonjwa cha Johns Hopkins.
Marekani ndio imerekodi vifo vingi duniani vinavyohusiana na ugonjwa huo hatari wa COVI-19, ugonjwa ambao ulikuwa na athari kwenye uchaguzi wa urais kati ya Joe Biden na Donald Trump Jumanne pamoja na matokeo yake.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.