MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Marekani 2020: Watu kadhaa wakamatwa wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi

Maandamano mengine yalifanyika huko New York, ambapo polisi inasema inawashikilia karibu watu 50, na pia huko Atlanta, Detroit na Oakland, ambapo waandamanaji walidai kwamba shughuli za uhesabuji wa kura ziendelee bila kizuizi.
Maandamano mengine yalifanyika huko New York, ambapo polisi inasema inawashikilia karibu watu 50, na pia huko Atlanta, Detroit na Oakland, ambapo waandamanaji walidai kwamba shughuli za uhesabuji wa kura ziendelee bila kizuizi. REUTERS

Polisi inawashikia watu kadhaa tangu jana usiku waliokamatwa wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi leo Alhamisi huko Portland, Oregon, ambapo Gavana Kate Brown aliwataka Walinzi wa Kitaifa kukomesha kile alichokiita "ghasia za jumla".

Matangazo ya kibiashara

Maandamano mengine yalifanyika huko New York, ambapo polisi inasema inawashikilia karibu watu 50, na pia huko Atlanta, Detroit na Oakland, ambapo waandamanaji walidai kwamba shughuli za uhesabuji wa kura ziendelee bila kizuizi.

"Maandamano yote ambayo yametangazwa kuwa ya ghasia yalifanyika katikati mwa jiji. Tumewakamata watu kumi," msemaji wa polisi ya Portland amesema katika taarifa, kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Wanaharakati wa Kulinda Matokeo (Protect the Result), kundi linalojumuisha mashirika na vyama vya wafanyakazi 165, wametabiri kutokea kwa matukio kama hayo zaidi ya mia moja nchini kote Marekani kati ya Jumatano na Jumamosi.

Timu ya kampeni ya Donald Trump, ambayo inadi zoezi la uhesabuji wa kura liligubikwa na udanganyifu mkubwa, inataka kusitishwa kwa zoezi hilo katika majimbo kadhaa ambapo mpizani wake Joe Biden anaongoza.

Huko Phoenix, Arizona, wafuasi wa rais aliye madarakani, ambao wengine walikuwa wamejihami kwa silaha, walikusanyika nje ya kituo cha kupigia kura baada ya uvumi usio na msingi kwamba kura za Donald trump zilipuuzwa kwa makusudi.