MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya zaidi 120,000 vyathibitishwa nchini Marekani

Marekani imerekodi visa vipya 120,276 zivyothibitishwa vya maambukizi ya virisi vya Corona, kulingana na takwimu za shirika la habari la REUTERS, ikiwa ni rekodi ya kila siku na siku ya pili mfululizo ya zaidi ya maambukizi 100,000.

Marekani ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani.
Marekani ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani. Barry Riley/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona limeripotiwa katika mikoa yote nchini Marekani, na maambukizi zaidi ya kila siku yaliripotiwa katika majimbo 20 siku ya Alhamisi.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.