MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Donald Trump adai 'uchaguzi uligubikwa na wizi'

Kituo cha kupigia kura huko Durham, North Carolina Novemba 3, 2020.
Kituo cha kupigia kura huko Durham, North Carolina Novemba 3, 2020. REUTERS/Jonathan Drake

Nani atachaguliwa kuwa rais mpya wa Marekani kati ya rais anaye maliza muda wake kutoka chama cha Republican Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, haya ni maswali ambayo wengi wanajiuliza Marekani na katika nchi mbalimbali duniani.

Matangazo ya kibiashara

►Bado halijajulikana jina la rais mpya wa Marekani. Joe Biden hata hivyo anaongoza kwa kura 264 za wajumbe maalumu dhidi ya 214 ambazo kufikia sasa amepata Donald Trump.

►Donald Trump ameshinda katika jimbo la Florida, jimbo muhimu, lakini pia Texas, jimb ambalo ni ngome ya kihistoria ya chama cha Republican lakini chama cha Democratic kilitarajia kushinda. Biden, kwa upande mwingine, ameshinda huko Arizona (RFI imepata takwimu hizi kutoka shirika la habari la Associated Press, lakini vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani vinabaini kuwa bado ni mapema sana kusema kuwa Joe Biden ameibuka mshindi katika jimbo la Arizona lenye wajumbe maalumu 11), jimbo ambalo pia ni ngome ya kihistoria cha chama cha Republican, lakini pia huko Wisconsin, jimbo ambalo lilimpigia kura Trump mnamo mwaka 2016, sawa na jimbo la Michigan.

►Matokeo ya majimbo haya mawili yanatarajiwa kutangazwa: Pennsylvania na Nevada ambapo Biden yuko mbele kidogo na ambapo anatarajia wajumbe sita pekee ili aweze kiupata ushindi wa uchaguzi huu wa urais.

►Donald Trump tayari ametangaza kuwa atafungua kesi mahakamani ili kuzuia zoezi la uhesabuji wa kura, akishtumu kuwa uchaguzi huo umegubikwa na udanganyifu mkubwa. Katika hotuba yake katika Ikulu ya White siku ya Alhamisi saa 6:45 jioni (saa za Marekani), rais anayemaliza muda wake alirelea kauli yake kwamba angelishinda uchaguzi wa urais wa Marekani, ambao chama cha Democratic kinajaribu "kumwibia", bila ushahidi wowote thabiti.

Hotuba hii, ambayo vituo kadhaa vya habari vya Marekani viliamua kukatiza kwa sababu ya madai yake ambayo hayana msingi, imekosolewa vikali, hata katika kambi yake.