MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Marekani 2020: Biden aongoza Pennsylvania na Gerogia, zoezi la uhesabuji kura laendelea

Joe Biden hatimae anaongoza kwa kura ambazo zimehesabiwa katika majimbo yenye ushindani mkali ya Georgia na Pennsylvania.

Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden.
Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden. REUTERS/Alan Freed
Matangazo ya kibiashara

Katika jimbo la Pennsylvania Joe Biden anaongoza kwa 49.4% ya kura dhidi ya 49.3% ya Donald Trump wakati 95% ya jumla kura zilizohesabiwa, kulingana na shirika la Edison Research.Hii

Hii inaonesha kuwa Joe Biden anaongoza kwa kura 5,587 na zoezi la uheshabuji wa kura linaendelea, shirika la Edison Utafiti limebaini.

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje katika jimbo la Georgia, Brad Raffensberger, ametangaza kwamba jimbo hilo litahesabu upya kura zake za urais.

Brad Raffensberger amebaini kwamba kura 4169 hazijahesabiwa na kwamba kura 8000 za wanajeshi bado zimo katika barua na kwamba sitahesabiwa zitakapowasili mwisho wa siku.

Hata hivyo Joe Biden amempiku Donald Trump katika mji wa Georgia.

Joe Biden aliye na umri wa miaka 77 na ambaye pia ni makamu wa zamani wa rais huenda akawa rais mpya ikiwa atashinda kura katika jimbo la Pennsylvania au kwa kushinda majimbo mawili kati ya Georgia, Nevada na Arizona.