MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Donald Trump: Biden hapaswi 'kushangilia ushindi kinyume cha sheria'

Joe Biden na Donald Trump,Septemba 29, 2020, wakati wa mdahalo wa kwanza wa televisheni kabla ya uchaguzi wa urais, Novemba 3, 2020.
Joe Biden na Donald Trump,Septemba 29, 2020, wakati wa mdahalo wa kwanza wa televisheni kabla ya uchaguzi wa urais, Novemba 3, 2020. REUTERS/Carlos Barria/Leah Millis

Rais wa Marekani anaye maliza muda wake Donald Trump amesema Ijumaa usiku kwamba Joe Biden hapaswi kudai ushindi kwa njia "haramu", wakati mpinzani wake kutoka chama cha Democratic anaonekana kuwa karibu sana na ushindi wa uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

"Joe Biden hapaswi kudai ameibuka mshindi wa uchaguzi wa urais kinyume cha sheria," rais Donald Trump ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter.

"Nitaweza hata mimi kudai ushindi. Utaratibu wa kisheria umeanza tu!", ameongeza.

Makamu wa rais wa zamani wa Barack Obama ambaye ni mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden amezungumza na umma wa Wamarekani na kutaja tena vipaumbele vyake katika kipindi hiki akiashiria ushindi wa urais.

Kufikia sasa hakuna hakuna mshindi wa uchaguzi huo wa urais ambaye ameishatangazwa mshindi.

Joe Biden amempiku Donald Trump katika mji wa Georgia .

Na huku matokeo ya kura yakitolewa, Biden amechukua uongozi dhidi ya Trump katika jimbo la Pennsylvania.

Georgia yenye wajumbe 16 inatosha kumfanya Biden kupata matokeo sawa na Trump katika idadi ya wajumbe, huku akisubiri matokeo maengine kutoka majimbo mengine.