MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Marekani 2020: Joe Biden aashiria ushindi wake katika uchaguzi wa urais

Joe Biden anaelekea kwenye hatua ya kushinda kinyang'anyiro cha urais dhidi ya Donald Trump, ambaye ameendelea kudai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na 'udanganyifu mkubwa'.

Joe Biden mgombea wa urais wa chama cha Democratic.
Joe Biden mgombea wa urais wa chama cha Democratic. AP Photo/Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa hakuna mshindi wa uchaguzi huo ambaye ameishatangazwa, Soika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, kutoka chama cha Democratic amebaini kwamba ni "dhahiri" Joe Biden "ataibuka mshindi wa uchaguzi wa urais".

Wakati huo huo rais anaye maliza muda wake Donald Trump amesema Ijumaa usiku kwamba Joe Biden hapaswi kudai ushindi kwa njia "haramu", wakati mpinzani wake kutoka chama cha Democratic anaonekana kuwa karibu sana na ushindi wa uchaguzi wa urais.

Hata hivyo zoezi la uhesabuji wa kura bado linaendelea, lakini makamu mgombea wa chama cha Democratic anaongoza katika jimbo la Pennsylvania tangu Jumanne, na sasa yuko mbele ya rais kutoka chama cha Republican kwa zaidi ya kura 13,000.

Hakuna media yoyote ambayo bado imeelezea ushindi huo kwa mmoja wa wagombea wawili katika jimbo hili kaskazini mashariki mwa viwanda nchini ambayo ina thamani ya wapiga kura 20, alishinda na Donald Trump mnamo 2016.

Ikiwa Joe Biden atapata ushindi huko Pennsylvania, atakuwa rais wa 46 wa Marekani, bila kujali matokeo ya uchaguzi katika majimbo mengine.