MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yavuka milioni 10 Marekani

Marekani imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni ambapo idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona imezidi kizingiti cha watu milioni 10, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la REUTERS, kupitia takwimu rasmi.

Kwa siku kumi zilizopita, takriban visa vipya milioni moja vya maambukizi vimethibitishwa nchini Marekani, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha kuenea kwa janga hilo tangu kesi ya kwanza kuthibitishwa katika jimbo la Washington karibu siku 300 zilizopita.
Kwa siku kumi zilizopita, takriban visa vipya milioni moja vya maambukizi vimethibitishwa nchini Marekani, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha kuenea kwa janga hilo tangu kesi ya kwanza kuthibitishwa katika jimbo la Washington karibu siku 300 zilizopita. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Marekani inaendelea kukabiliwa na mlipuko mpya wa janga la COVID-19.

Marekani ilivuka kizingiti hiki siku ambayo idadi ya visa vya maambukizi ulimwenguni ilizidi milioni 50.

Kwa siku kumi zilizopita, takriban visa vipya milioni moja vya maambukizi vimethibitishwa nchini Marekani, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha kuenea kwa janga hilo tangu kesi ya kwanza kuthibitishwa katika jimbo la Washington karibu siku 300 zilizopita.

Zaidi ya visa 130,000 vya maambukizi viliripotiwa siku ya Jumamosi pekee.

Janga hilo limesababisha zaidi ya vifo 237,000 nchini Marekani.