MAREKANI-URUSI-CHINA-USHIRIKIANO

Marekani 2020: China, Urusi wakataa kumpongeza Joe Biden kabla ya matokeo rasmi

China na Urusi zimesema zinasubiri matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais wa Marekani kabla ya kumpongeza Joe Biden, aliyeibuka mshindi. Wakati huo huo timu za Donald Trump zimeenndelea kuwasilisha malalamiko mahakamani ili zoezi la uhesabuji lirejelewe upya katika majimbo kadhaa yenye uamuzi.

Joe Biden, wakati alikuwa makamu wa rais, alikutana na rais wa China Xi Jiping, Septemba 25, 2015 huko Washington (picha ya kumbukumbu).
Joe Biden, wakati alikuwa makamu wa rais, alikutana na rais wa China Xi Jiping, Septemba 25, 2015 huko Washington (picha ya kumbukumbu). PAUL J. RICHARDS / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Siku ya Jumamosi jioni Joe Biden alijitangaza kuwa rais wa 46 wa Marekan baada ya kuzidisha kizingiti cha kura 270 za wajumbe maalumu wenye uamuzi katika uchaguzi wa urais nchini Marekani. Kufikia sasa Donald Trump amekataa kukubali kushindwa.

Viongozi wengi wa kimataifa, pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na viongozi wengine wa kisiasabarani Ulaya, walituma pongezi zao kwa rais mteule, lakini rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamekaa kimya.

"Tuunajua kwamba Bw. Biden ametangaza ushindi wake," msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin almesema katika mkutano na waandishi wa habari. "Tunaelewa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa Marekani yataamuliwa kulingana na sheria na taratibu za Marekani," ameongeza.

Mnamo mwaka 2016, Xi Jinping alituma pongezi zake kwa Donald Trump siku moja baada ya uchaguzi.Kwa upande wake, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema katika mkutankusubiri matokeo rasmi yatangazwe kabla ya kutoa maoni.