MAREKANI-TRUMP-USALAMA

Donald Trump amfuta kazi mkuu wa Pentagon Mark Esper

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amefutwa kazi na Donald Trump Jumatatu, Novemba 9.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amefutwa kazi na Donald Trump Jumatatu, Novemba 9. AP Photo/Alex Brandon

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kumfuta kazi Waziri wake wa Ulinzi Mark Esper, ambaye nafasi yake itachukuliwa na mkurugenzi wa kituo cha kitaifa cha kupambana na ugaidi, Christopher Miller.

Matangazo ya kibiashara

Kama kawaida yake, Donald Trump ametangaza uamuzi wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, mwandishi wetu huko Washington Anne Corpet ameripoti.

Hii ni desturi iliyoanzishwa na rais huyu ambaye ameshindwa katika uchaguzi wa Novemba 3 na mpizani wake Joe Biden kutoka chama cah Democratic.

Amesema kwenye Twitter kwamba Christopher Miller anachukua nafasi hiyo mara moja kama mkuu wa Pentagon.

“Chris atafanya kazi kubwa! Mark Esper amefutwa kazi. Ninamshukuru kwa kazi yake ”, rais wa Marekani Donald Trump ameandika ujumbe mfupi wa maneno kwenye ukurasa wake wa Twitter, siku mbili baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa alishindwa kufanya vizuri katika uchaguzi wa urais.