PERU-SIASA

Peru: Rais Martin Vizcarra atimuliwa na Bunge

Rais wa Peru aliyeondolewa madarakani Martin Vizcarra ametangaza kwamba ataachia ngazi Jumatatu, Novemba 9 jioni.
Rais wa Peru aliyeondolewa madarakani Martin Vizcarra ametangaza kwamba ataachia ngazi Jumatatu, Novemba 9 jioni. AP Photo/Martin Mejia

Miezi miwili baada ya jaribio la kwanza, Bunge la Peru limeidhinisha kufutwa kazi kwa Rais Martin Vizcarra likimshtumu "kutokuwa na uwezo wa kudumu wa maadili" kufuatia tuhuma za ufisadi, miezi michache tu kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Aprili 2021.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mjadala wa uliyodumu saa 5, wabunge wa Peru walipiga kura Jumatatu jioni kumtimua rais Martin Vizcarra kwa kura 105, zaidi ya kura 87 zinazohitajika kati ya 130 kwa kumwondoa mamlakani kiongozi wa nchi.

Rais Martin Vizcarra anashukiwa kupokea rushwa kutoka kwa kampuni za ujenzi wakati alikuwa gavana wa mkoa wa Moquegua kati ya mwaka 2011 na 2014.

Jaribio la kwanza la kushtakiwa na bunge lilishindwa mnamo mwezi Septemba, baada ya wabunge 32 kupipiga kura.

Kufuatia kura hiyo mpya, msemaji wa chama cha Umoja kwa Peru , mojawapo ya vyama vilivyo anzishamchakato wa wa kumtimua rais huyo, amekaribisha uamuzi wa Bunge kwa niaba ya kupambana na ufisadi.