MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 100,000 zathibitishwa Marekani kwa siku ya saba mfululizo

Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka nchini Marekani. REUTERS

Marekani imeendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona. Jumanee wiki hii visa vipya 100,000 vya maambukizi vilithibitishwa kwa siku ya saba mfululizo, kulingana na takwimu za shirika la habari la REUTERS, kupitia takwimu rasmi.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo vipya imefikia kiwango cha juu cha kila siku tangu mwezi Agosti.

Wakati majimbo machache yanaendelea kukusanya takimu za walioambukizwa virusi vya Corona, angalau visa 134,000 vipya vilipotiwa Jumanne mchana. Wiki iliyopita, visa vipya 120,000 viliripotiwa kila siku.

Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka.

Kwa kukabiliana na mlipuko huu mpya wa janga hilo, majimbo kadhaa ikiwa ni pamoja na California yameimarisha vizuizi vya kiafya, kuagizwa tena kufungwa kwa mikahawa na kumbi za michezo.