MAREKANI-SIASA-UCHUMI

Joe Biden amteua mshauri wake Ron Klain kama mkurugenzi wake wa baadaye White House

Rais mteule wa Marekani anaendelea na mchakato wa kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchina amemteua mmoja wa washirika wake wa karibu, ambaye hapo awali alifanya kazi naye wakati alikuwa makamu wa rais, kuongoza ofisi yake.

Ron Klain pamoja na Joe Biden, wakati huo makamu wa rais, mwaka 2014, wakati alikuwa mratibu wa mapambano dhidi ya Ebola.
Ron Klain pamoja na Joe Biden, wakati huo makamu wa rais, mwaka 2014, wakati alikuwa mratibu wa mapambano dhidi ya Ebola. REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden amemteua Ron Klain, kada wa chama cha Democratic mwenye uzoefu mkubwa, kuwa mkurugenzi katika Ikulu ya White House, amesema katika taarifa.

"Ron amekuwa muhimu sana kwangu kwa miaka mingi ambapo tumefanya kazi pamoja," rais mteule wa Marekani amebaini.

"Uzoefu wa muda mrefu na tofauti wa Ron Klain na uwezo wa kufanya kazi na watu kutoka tabaka mbalimbali za kisiasa ndio hasa ninachohitaji kwa mkurugenzi wa Ikulu ya White House wakati kwa sasa tunakabiliwa na mgogorona tuunganishe tena nchi yetu, ”ameongeza Joe Biden.

Mshirika wa muda mrefu

Ron Klain, 59, pia alifanya kazi na Joe Biden wakati alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Seneti kuhusu masuala ya sheria. Baadaye alikuwa mkurugenzi wa ofisi ya Makamu wa Rais Al Gore. Chini ya utawala wa Barack Obama, Ron Klain aliratibu, katika ikulu ya White House, mapambano dhidi ya mgogoro wa Ebola mnamo 2014.

Ron Klain amesema kuwa uteuzi huu ni "heshima ya maisha" kuteuliwa kwa wadhifa huu. "Ninatarajia kumsaidia yeye na Makamu wa rais Mteule kuleta pamoja timu yenye uzoefu kufanya kazi katika ikulu ya White House, ili kutuonyesha mipango yao ya kutaka mabadiliko, na kutafuta kuziba mgawanyiko katika nchi hii, ”ameongeza.

Chaguo la Ron Klain limekaribishwa na wafuasi wa chama cha Democratic. Seneta Elizabeth Warren aliita uteuzi huo kama "chaguo bora" kwa sababu "anaelewa kiwango cha mgogoro wa kiafya na kiuchumi na ana uzoefu wa kuongoza utawala huu ujao."