Marekani: Ukosefu wa ushahidi, mawakili wa Trump wakabiliwa na usumbufu mahakamani
Siku moja baada ya ushindi wa Joe Biden kutangazwa, Donald Trump aliahidi kupinga matokeo haya mahakamani akishutumu kwamba uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa.
Imechapishwa:
Rais Donald Trump kwa sasa anakabiliwa na matatizo kuhusu kesi yake mahakamani: Mawakili wake hawawezi kuthibitisha udanganyifu wa uchaguzi ambao wanadai kuwa uligubika uchaguzi huo wa Novemba 3.
Taratibu zao zote zimekataliwa na majaji wa Marekani. Kkukosekana kwa ushahidi mahakamani, ni aibu kwa mawakili wa Donald Trump.
Mojawapo ya masikitiko makubwa ni kutoka katika mahakama ya shirikiso huko Pennsylvania, wakati kambi ya Trump ilipotaka mahakama isitishe zoezi la uhesabuji wa kura kwa sababu waangalizi wa chama cha Republican walidaiwa kuzuiliwa kuingia katika kituo cha kupigia kura.
Wakati wa kesi hiyo ikisikilizwa, wakili wa kambi ya Donald Trump alikosa ushahidi wa kuthibitisha tukio hili. Kinyume chake, jaji alimthibitishia kwamba waangalizi wa chama cha Republican sio tu walikuwepo katika kituo hicho cha kupigia kura lakini pia walikuwa wengi hata zaidi ya mara mbili kwa wale wa chama cha Democratic.
"Pole sana, lakini shida yako ni nini hasa?" aliuliza jaji, ambaye aliteuliwa na rais wa kutoka chama cha Republican.
Uvumi
"Mfano mwingine ni katikamahakama ya shirikisho huko Detroit, katika jimbo la Michigan ambapo mawakili kutoka kambi ya Trump walitoa malalamiko kwa sababu kura zilisemekana kuthibitishwa siku mbili baada ya tarehe ya mwisho iliyotolewa kisheria. Chanzo chao: mwangalizi ambaye hakushuhudia moja kwa moja tukio linalodaiwa. "Ok, hiyo ndio naita uvumi," jaji alihitimisha.
Katika hatua hii, malalamiko kadhaa ya udanganyifu na makosa yaliyowasilishwa na Ikulu ya White House yamekataliwa. Hakuna kilichoonekana kuwa sahihi kwa jaji ili kuidhinisha kufungua uchunguzi.