PERU-MAANDAMANO-SIASA

Peru: Maandamano yaendelea baada ya kufutwa kazi kwa Vizcarra

Waandamanaji waliandamana katika mitaa mbalimbali kupinga uamuzi wa Bunge, na wengi wao walikamatwa na polisi baada ya makabiliano.
Waandamanaji waliandamana katika mitaa mbalimbali kupinga uamuzi wa Bunge, na wengi wao walikamatwa na polisi baada ya makabiliano. REUTERS

Kaimu Rais wa Peru Manuel Merino ametoa wito kwa watu kuwa watulivu baada ya maandamano kuzuka nchini humo kufuatia kufutwa kazi kwa Martin Vizcarra.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, Bunge la Peru lilimtimuwa mamlakani rais Martin Vizcarra anayekabiliwa na kesi ya mashtaka dhidi ya ufisadi.

"Tunawaheshimu watu wenye maoni tofauti na yetu, lakini tunatoa wito wa utulivu na uwajibikaji ili kujieleza kisiasa kuzingatiwe kwa utulivu na bila vurugu," Manuel Merino amesema alipokuwa akilihutubia taifa.

Peru inakabiliwa na mgogoro huu wa kisiasa wakati inapojaribu kuijiinua kiuchumi, hali iliyosababishwa na mgogoro wa kiavya kutokana na janaga la Corona.

Waandamanaji waliandamana katika mitaa mbalimbali kupinga uamuzi wa Bunge, na wengi wao walikamatwa na polisi baada ya makabiliano.

Alhamisi jioni, maelfu ya wakazi wawaliandamana katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Lima, wakiwa na sufuria.

"Tumechoka na ufisadi, ndio sababu niko hapa, nikipiga kelele na sufuria yangu," alisema Rosario Mendoza, mmoja wa waalimu ambaye alikuwa akiandamana katika mji mkuu wa Lima. "Si Bunge wala rais waliyemchagua haniwakilishi mimi," ameongeza.

Jumuiya ya maedeleo ya nchi za Amerika (OAS) imeelezea wasiwasi wake juu ya "mzozo huu mpya wa kisiasa nchini Peru", na imetoa wito kwa Mahakama ya Katiba kuingilia kati.