PERU-SIASA

Peru: Wabunge washindwa kufikia makubaliano ya kupata mrithi wa Manuel Merino baada ya kujiuzulu

Manuel Merino alishikilia wadhifa wake kwa muda wa wiki moja kama rais wa mpito wa Peru. Alichukua nafasi ya rais Martín Vizcarra baada ya kuondolewa madarakani na bunge Jumatutu wiki iliyopita kwa madai ya hongo, ambayo aliyakanusha.

Raia wa Peru wakitoa heshima zao kwa vijana wawili waliouawa wakati wa maandamano wakipinga kuftimuliwa kwa rais Martin Vizcarra.
Raia wa Peru wakitoa heshima zao kwa vijana wawili waliouawa wakati wa maandamano wakipinga kuftimuliwa kwa rais Martin Vizcarra. Luka Gonzales/AFP
Matangazo ya kibiashara

Lakini maandamano ambayo yaliongezeka na kukandamizwa kikatili yalimfanya apoteze uungwaji mkono, hatua ambayo ilikuwa imebaki. Alijiuzulu Jumapili hii, Novemba 15.

Wajumbe wa Bunge la Peru hawakuweza kufikia makubaliano ya kumchagua rais wao na wamakamu watatu wa rais, kulingana na ripoti ya mwandishi wetu huko Lima, Eric Samson. Walakini, kulikuwa na orodha moja tu, lakini wabunge 45 tu ndio walipiga kura ya "Ndio" wakati kulikuwa kunahitajika wabunge 60. Vyama vinatakiwa kuwasilisha orodha mpya mnamo Novemba 17.

Uchaguzi huu ulikuwa muhimu zaidi kwa kuwa, kulingana na Katiba, rais wa baadaye wa bunge la Congress moja kwa moja anatakiwa kuwa rais mpya wa jamhuri. Jina la mwanzo kwenye orodh hiyo lilikuwa la mbunge Rocio Silva, mmoja wa wachache ambao hawakupiga kura ya kumtimuwa Martin Vizcarra.

Hata hivyo yule ambaye alifikiri kuwa atakuwa rais mwanamke wa kwanza wa Peru hakuchaguliwa, labda kwa sababu uchaguzi wake ungewalazimisha wabunge wengi kukubali kuwa kutimuliwa kwa Martin Vizcarra hakukuwa sahihi.

Martin Vizcarra hajakata tamaa ya kurudi madarakani. "Ni Mahakama ya Katiba ambayo lazima iamue ikiwa uamuzi wa Bunge wa kuniondoa madarakani ulikuwa halali," amesema. Tunaiwomba isingoje hadi Jumatano [Novemba 18] na ichukuwe uamuzi mara moja. Hatuwezi kusubiri. Mahakama lazima ikutane haraka na kuchukuwa uamuzi wake mara moja, ameongeza Martin Vizcarra.