Ndege aina ya Boeing 737 MAX kuanza kuruka tena
Marekani imeruhusu ndege aina ya Boeing 737 MAX kuruka tena, baada ya karibu miaka miwili kutofanya safari yoyote kufuatia ajali mbili zilizoua watu 346 katika kipindi cha miezi mitano.
Imechapishwa:
Ndege hii, ambayo ilitengenezwa na kampuni ya Boeing nchini Marekani kabla ya mgogoro huo, hata hivyo, haitoruhusiwa mara moja katika anga za nchi mbalimbali dunia.
Mamlaka za anga kutoka nchi mbalimbali wameamua kufanya ukaguzi wa ndege hiyo wao wenyewe.
Shirika la Usafiri wa Anga nchini Marekani (FAA), pia limebainisha katika taarifa yake Jumatano wiki hii kwamba inatarajia kwanza kuidhinisha mafunzo muhimu kwa marubani kabla ya ndege yoyote aina ya Boeing 737 MAX kupaa juu ya anga la Marekani.
Hata hivyo shirika la ndege la Marekani, American Airlines, tayari limepanga safari kwa kutumia ndege hiyo mwishoni mwa mwezi Desemba.
Nchi nyingi duniani zilisitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.