MEXICO-CORONA-AFYA

Corona yauawa zaidi ya 100,000 Mexico

Mamlaka ya afya nchini Mexico imeonya kuwa idadi halisi ya watu waliofariki dunia kutokana na Corona huenda ikazidi idadi ya vifo vilivyorekodiwa.
Mamlaka ya afya nchini Mexico imeonya kuwa idadi halisi ya watu waliofariki dunia kutokana na Corona huenda ikazidi idadi ya vifo vilivyorekodiwa. REUTERS

Mexico imepitisha kizingiti cha vifo 100,000 kutokana na janaga la Corona, siku chache baada ya kufikia visa milioni moja vya maambukizi, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Afya imeripoti ongezeko la vifo 576 katika muda wa saa 24 kwa jumla ya vifo 100,104 tangu kuzuka kwa janga hilo.

Wizara hiyo pia imeongeza kwenye orodha yake vifo vipya 15,000 vilivyochukuliwa kuwa "vyevye mashaka."

Mamlaka ya afya imeonya kuwa idadi halisi ya watu waliofariki dunia kutokana na Corona huenda ikazidi idadi ya vifo vilivyorekodiwa.