MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Giuliani: Trump anaweza kuibuka mshindi wa uchaguzi wa urais Marekani

Wakili wa Donald Trump katika mkutano wake na waandishi wa habari huko Washington mnamo Novemba 19, 2020.
Wakili wa Donald Trump katika mkutano wake na waandishi wa habari huko Washington mnamo Novemba 19, 2020. AP - Jacquelyn Martin

Rais wa Marekani anaendelea na vita vyake kujaribu kupindua matokeo ya uchaguzi ambayo yanaonyesha kuwa ameangushwa na mpinzani wake Joe Biden kutoka chama cha Democratic.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump amekataa kukubali kushindwa licha ya matokeo kuonyesha kuwa Joe Biden anaongozwa kwa kura nyingi.

Utaratibu alioanzisha Donald Trump na kambi yake kwa kuwasilisha malalamiko yao mbele ya vyombo vya sheria, umeonga mwamba, lakini Donald Trump hakubali kuacha.

Alhamisi wiki hii wakili wake alidai bila ushahidi wowote kwamba ushindi wa mteja wake unawezekana kwa wakati wowote.

"Kulikuepo na udanganyifu mkubwa katika majimbo mbalimbali," alisema Rudolf Giuliani kabla ya kubaini njama kubwa iliyopangwa na chama cha Democratic.

"Hii inaonesha mpango uliobuniwa kutoka eneo fulani kuandaa udanganyifu huu hasa katika miji mikubwa inayodhibitiwa na chama cha Democratic. Ni mpango ambao unatoka moja kwa moja kwa Chama cha Democratic na yote haya yalipangwa na mgombea urais kutoka chama hicho. Ni wazi, "alisema mwanasheria na mshauri wa Donald Trump.

"Tutakuwa kama Venezuela"

Bila kutoa ushahidi wowote isipokuwa ushuhuda wa kipekee wa mfanyakazi wa jiji la Detroit ambaye anadaiwa alishuhudia wizi huo, wakili wa rais amesisitiza: "Ikiwa hakuana hatua zitakazo chukuliwa, tutakuwa kama Venezuela. Hatuwezi kuwaacha watufanyie hivi. Hatuwezi kukubali mafisadi hawa waibe uchaguzi wa raia wa Marekani. Walimchagua Donald Trump, hawakumchagua Joe Biden. "

Vituo vya Televisheni vilikata haraka matangazo ya Rudolf Giuliani, isipokuwa kituo cha Fox News.