MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Donald Trump aridhia kuanza kwa mchakato wa kumkabidhi madaraka Joe Biden

Donald Trump, Novemba 20, 2020.
Donald Trump, Novemba 20, 2020. MANDEL NGAN AFP

Donald Trump ametangaza mapema Jumatatu jioni, Novemba 24, kwamba ameridhia ufunguzi wa mchakato wa kumkabidhi madaraka mrithi wake Joe Biden kutoka chama cha Democrtaic, zaidi ya wiki mbili baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Idara ya serikali ya Marekani inayoratibu shughuli ya kubadilishana madaraka, imempatia rais mteule Joe Biden idhini ya kuendelea na mchakato wa kukabidhiana madaraka huku Trump naye akionekana kukubali kutoa ushirikiano

Trump amekiri kuwa umefika muda sasa kwa taasisi hiyo kufanya "kinachohitajika" na kaandika katika Twitta kwamba ameielekeza timu yake kutoa ushirikiano katika mchakato wa kukabidhiana madaraka.

Wakati huo huo Timu ya Bwana Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati rais mteule anajiandaa katika sherehe za kuapishwa Januari 20.

Rais anayemaliza muda wake Donald Trump kutoka chama cha wa Republican, hata hivyo, amejizuia kutambua moja kwa moja ushindi wa Joe Biden, huku akiahidi kuendelea na "mapambano ya haki" wakati anaendelea kuwasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama mbalimbali nchini humo, bila mafanikio yoyote, kujaribu kuonyesha udanganyifu wakati wa uchaguzi wa urais wa Novemba 3 .

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".