MAREKANI-CORONA

Coronavirus: Zoezi la kutoa chanjo kuanza wiki ijayo Marekani

Marekani kuanza kusambaza chanjo kuanzia mwezi ujao
Marekani kuanza kusambaza chanjo kuanzia mwezi ujao Photo AP / Hans Pennink

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa zoezi la kutoa chanjo dhidi ya Corona litaanza wiki ijayo na kuendelea wiki inayofuata.  

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano kwa njia ya video wakati wa hafla ya Thanksgiving na wanajeshi wa Marekani waliopelekwa katik nchi za kigeni, Alhamisi wiki hii, Donald Trump alisema chanjo hiyo itatumwa kwa wafanyakazi ambao wako kwenye mstari wa mbele dhidi ya mgogoro wa kiafya, wafanyakazi wa afya na wazee.

 

Marekani inaendelea kusakamwa na ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Ugonjwa huo hatari wa COVID-19 umesababisha vifo vingi nchini Marekani na idadi ya maambukizi imeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali nchini humo.

 

Idadi ya maambukizi imekuwa ikipanda katika mataifa ya Amerika ya kusini . Brazil ikiwa na uchumi mkubwa katika eneo hilo, ina karibu kesi milioni 1.5 zilizothibitishwa, ikiwa ni ya pili tu kutoka Marekani.