MAREKANI-COVID 19

Covid-19: Mikusanyiko ya umma yapigwa marufuku Los Angeles kwa wiki tatu

Ugonjwa wa Covid 19 tayari umeua maelfu ya raia wa Marekani
Ugonjwa wa Covid 19 tayari umeua maelfu ya raia wa Marekani Fabrice COFFRINI / AFP

Mamlaka ya afya huko Los Angeles (California), nchini Marekani, imetangaza marufuku ya mikusanyiko ya umma na ya kibinafsi, kwa muda wa wiki tatu.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umechukuliwa kutokana na kuongezeka visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19.

 

Katika taarifa, mamlaka imetangaza kwamba "mikusanyiko yoyote ya umma na ya kibinafsi ya watu wasio kuwa wa familia moja ni marufuku, isipokuwa huduma za kidini na maandamano".

 

Hatua hii itaanza kutumika kuanzia Jumatatu, Novemba 30 na itatumika kwa kipindi cha wiki tatu.

 

Nchini Merika, kunaripotiwa zaidi ya visa milioni 12.8 vya maambukizi ya virusi vya Corona na zaidi ya vifo 263,000 kutokana na virusi hivyo. Marekani inaoongoza kwa vifo kutokana na COVID-19 duniani, ikifuatiwa na Brazil (vifo 171,000 ) na India (vifo 135,000). Janga hilo limeuwa watu wasiopungua milioni 1.4 duniani.