Trump: Sintobadilisha msimamo wangu" kuhusu wizi wa kura

Rais wa Marekani, Donald Trump, Novemba 20, 2020.
Rais wa Marekani, Donald Trump, Novemba 20, 2020. MANDEL NGAN AFP

Rais a,naye maliza muda wake nchini Marekani Donald Trump amesema 'kamwe hatobadilisha msimamo wake" juu ya mashtaka yake bila uthibitisho wa wizi wa kura, katika mahojiano yake ya kwanza ya runinga tangu Joe Biden kutangazwa msindi wa uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

"Hakuna mtu ambaye anaweza kunibadilisha mawazo yangu. Sintobadilisha mawazo yangu kwa kipindi cha miezi sita," rais Donald trump amekimbia kituo cha Fox News.

 

"Uchaguzi huu uligubikwa na wizi wa kura," amesema bila kutoa ushahidi wowote. "Tulishinda kwa kiasi kikubwa."

 

Kwa mahojiano yake ya kwanza ya runinga tangu kufanyika kwa uchaguzi wa urais Novemba 3, Bw.Trump amerejelea kwa dakika 45 mashtaka yake ya udanganyifu mkubwa mbao anadai ulisababisha anashindwa katika uchaguzi huo.

 

Licha ya shutuma za mara kwa mara za bilionea huyo wa Marekani, mawakili wake wameendelea kushindwa katika mahakama mbalimbali nchini marekani, wakijaribu kuonyesha jinsi uchaguzi huo wa urais uligubikwa na udanganyifu mkubwa.

 

"Tunajaribu kuonyesha ushahidi, lakini majaji hawaturuhusu," amesema Donald Trump. "Tunajaribu. Tuna ushahidi mwingi."

 

Akipuuzia uhuru wa mahakama, rais wa Marekani ameilalamikia Wizara ya Sheria na shirika la ujasusi la Marekani la FBI kutomuunga mkono.