Covid-19: Tume ya FDA kukagua ombi la Moderna Desemba 17
Imechapishwa:
Maabara ya Moderna imetangaza kuwa imewasilisha ombi la idhini ya dharura ya chanjo yake dhidi ya Covid-19 kwa mamlaka ya dawa ncini Marekani, Food and Drug Admnistration (FDA).
Moderna ni kampuni ya pili, baada ya Pfizer, kuwasilisha ombi kwa mamlaka ya FDA.
Mamlaka ya dawa nchini Marekani, kwa upande wake imetangaza kwamba tume yake ya ushauri inayosimamia chanjo na bidhaa zinazohusiana za kibaolojia (VRBPAC) itakutana mnamo Desemba 17 kuchunguza faili ya kampuni hiyo ya bioteknolojia.
Tume hii inatarajia kujadili ombi la kampuni ya Pfizer la Desemba 10.
Kulingana na Dk Moncef Slaoui, aliyeteuliwa na Donald Trump kuratibu maendeleo ya chanjo dhidi ya Covid-19, lengo la mamlaka hiyo ni kuweza kupeleka chanjo kwenye vituo vya chanjo katika muda wa saa 24 kulingana na idhini yake.
Jana Jumatatu kampuni ya Moderna ilitangaza kuwa itawasilisha maombi ya idhini ya uuzaji wa chanjo yake nchini Marekani na Ulaya, uwezo wake ukiwa umeonyesha ufanisi wa 94.1% katika elimu ya kliniki ya hali ya juu.