MAREKANI

Barr afutilia mbali madai ya wizi wa kura ya Donald Trump

Televisheni ikionesha matokeo ya wakati wa uchaguzi mkuu wa Marekani, Novemba 3.
Televisheni ikionesha matokeo ya wakati wa uchaguzi mkuu wa Marekani, Novemba 3. ion Night watch party and drag show, Tuesday, Nov. 3, 2020, in t

Mwanasheria mkuu nchini Marekani William Barr amesema Ofisi yake haijapata ushahidi wowote kuthibitisha madai ya rais Donald Trump kuwa aliibiwa kura wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Barr ambaye ni mshirika wa rais Trump , ni pigo kwa kiongozi huyo wa Marekani amabaye ameendelea kusisitiza kuwa aliibiwa kura na kukataa kutambua ushindi wa Joe Biden.

 

Mwanasheria huyo amesema baada ya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, hakuna ushahidi wowote uliojitokeza kuwa Trump aliibiwa kura.

 

Trump amekuwa akidai kuibiwa kura katika majimbo ya Pennyslovania, Gerogia na Wiscosin, lakini mawakili wake wameshindwa kuthibitisha hilo na kesi zake kutupiliwa mbali.

 

Rais mteule Biden ameendelea na maandalizi ya kuapishwa tarehe 20 mwezi Januari licha ya rais Trump kutotambua ushindi wake na ameendelea kufanya uteuzi wa watu watakaomsaidia kuongoza nchi.

 

Wiki moja iliyopita, rais Trump hata hivyo alisema kuwa ataondoka katika Ikulu ya White House iwapo Biden atathibitishwa na wajumbe wanaoamua mshindi wa Marekani kuwa alishinda, zoezi ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 14 mwezi huu.