JOE BIDEN-MAREKANI

Biden: Sitorejelea mkataba wa kibiashara kati ya Marekani na China

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden. Hapa ilikuwa ni Novemba 16, 2020.
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden. Hapa ilikuwa ni Novemba 16, 2020. AP Photo/Andrew Harnik

Joe Biden hatarejelea kwa sasa mkataba wa muda wa kibiashara uliofikiwa kati ya Donald Trump na China, rais mteule wa Marekani amenukuliwa na Gazeti la New York Times leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

"Sitachukua hatua yoyote ya haraka na hiyo inatumika kwa ushuru," Joe Biden amesema katika mahojiano na mwandishi wa Gazeti la New York Times. "Sitapunguza mamlaka yangu."

 

Kama sehemu ya mkataba huu wa kibiashara unaoitwa "awamu ya kwanza", uliosainiwa mwanzoni mwa mwaka huu, China imeahidi kuongeza angalau dola bilioni 200 (sawa na euro bilioni 166) kwa mwaka wa 2020 na 2021 kwa ununuzi wa bidhaa na huduma za Marekani.

 

Mkataba huu pia unaweka malipo ya kodi kwa 25% kwa bidhaa za China na vifaa vya viwandani vyenye thamani ya $ 250 bilioni vinavyoingizwa nchini Marekani na zaidi ya dola bilioni 100 bidhaa kutoka Marekani zinazoingia nchini China.

 

Kulingana na Joe Biden, ambaye anatarajia kuingia madarakani mnamo mwezi Januari, mkakati bora dhidi ya China kwanza ni kuiweka Marekani na washirika wake kwenye 'nafasi sawa".