MARKANI-DONALD TRUM

Uchaguzi Marekani 2020: Trump aapa kuendelea na utaratubu wa kisheria kudai atendewe haki

Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump. AP Photo/Ross D. Franklin

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine amedai kuwa aliibiwa kura, bila ya kutoa ushahidi wowote, madai ambayo yameendelea yameendelea kuwa gumzo nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia hotuba ya karibu dakika 40 iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii, Trump hakutambua ushindi wa rais mteule Joe Biden, hata baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali yake William Barr kusema kuwa hakuna ushahidi unaonesha kuwa wizi huo ulitokea.

Mapema wiki hii Mwanasheria mkuu nchini Marekani William Barr alisema Ofisi yake haijapata ushahidi wowote kuthibitisha madai ya rais Donald Trump kuwa aliibiwa kura wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Novemba.

Trump amekuwa akidai kuibiwa kura katika majimbo ya Pennyslovania, Gerogia na Wiscosin, lakini mawakili wake wameshindwa kuthibitisha hilo na kesi zake kutupiliwa mbali.

Rais mteule Biden ameendelea na maandalizi ya kuapishwa tarehe 20 mwezi Januari licha ya rais Trump kutotambua ushindi wake na ameendelea kufanya uteuzi wa watu watakaomsaidia kuongoza nchi.

Wiki moja iliyopita, rais Trump hata hivyo alisema kuwa ataondoka katika Ikulu ya White House iwapo Biden atathibitishwa na wajumbe wanaoamua mshindi wa Marekani kuwa alishinda, zoezi ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 14 mwezi huu.