MAREKANI-COVID19

Coronavirus: Wamarekani milioni 20 kupewa chanjo mwaka huu,

Idadi ya maambukizi inazidi kupanda Marekani wakati huu chanjo ikikaribia kuanza kutolewa.
Idadi ya maambukizi inazidi kupanda Marekani wakati huu chanjo ikikaribia kuanza kutolewa. Photo AP / Hans Pennink

Kulingana na mamlaka ya dawa Marekani, Food and Drug Administration (FDA), Wamarekani milioni 20 watapewa chanjo dhidi ya COVID-19 ifikapo mwishoni wa mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa mamlaka hiyo ya dawa nchini Marekani, Stephen Hahn akinukuliwa na shirika la habari la REUTERS, amekataa kutoa ratiba sahihi juu ya uthibitisho wa chanjo ya majaribio iliyotengenezwa na maambara kutoka Marekani ya Pfizer kwa ushirikiano na maambara kutoka Ujerumani ya BioNTech.

 

Hata hivyo amesema kuwa mamlaka hiyo itachukua hatua "haraka sana" baada ya kikao cha kamati ya ushauri kitakachofayika Desemba 10.

 

Mara tu FDA itakapoidhinisha chanjo hiyo, "nitakuwa wa kwanza kupewa chanjo na nitahimiza familia yangu kufanya hivyo," Stephen Hahn amesema katika mahojiano.

 

Ametangaza pia kwamba alikuwa na "mazungumzo ya kinai" katika Ikulu ya White House na Mkuu wa ofisi ya rais Mark Meadows kujadili ratiba ya chanjo.

 

Tovuti ya Axios imeripoti kwamba Stephen Hahn aliitwa Ikulu mapema wiki hii kuelezea ni kwanini chanjo kutoka Pfizer na BioNTech ilikuwa bado haijaidhinishwa nchini.

 

Stephen Hahn alisema hajazungumza na Rais mteule Joe Biden au kuwa na mawasiliano yoyote na timu yake, na kuongeza kuwa majadiliano juu ya usambazaji wa chanjo yanashughulikiwa na Idara ya Afya na Huduma za Binadamu.

 

Maafisa wengi wa Marekani wanasubiri idhini ya chanjo baada ya mkutano wa Desemba 10, ingawa afisa wa FDA hivi karibuni alisema uamuzi kama huo unaweza kuchukua wiki kadhaa.

 

Donald Trump, ambaye aliweka shinikizo kwa maabara, anaweza kurekodi ushindi wa mwisho pamoja na uuzaji wa chanjo hiyo wiki chache kabla ya kumkabidhi madaraka mrithi wake Joe Biden.