MAREKANI

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 200,000 vyathibitishwa Marekani,

Chanjo ya Covid 19.
Chanjo ya Covid 19. JOEL SAGET / AFP

Marekani imerekodi visa vipya 211,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona Alhamisi wiki hii na vifo vipya 2,858 vinavyohusiana na janga hilo, rekodi kwa siku moja, kulingana na takwimu rasmi.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa watu zaidi ya Milioni 14 wameambukizwa virusi vya Corona na vifo 275,000 vimeripotiwa, wakati idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini inazidi 100,000 nchini Marekani.

Wakati Wamarekani wengi walipuuzia maonyo ya afya wiki iliyopita kwa hafla ya Thanksgiving, wataalam wanahofia kuongezeka kwa mgogoro huo wa kiafya na huenda kukaripotiwa vifo 3,000 vya kila siku kwa miezi miwili ijayo.

Kutokana na hali hiyo kuendelea kuwa mbaya katika maeneo mbalimbali huko California, meya wa mji wa Los Angeles Jumatano aliagiza wakazi wote wa mji huo kubaki nyumbani.