MAREKANI

Biden kuja na mpango mpya wa mabilioni ya pesa

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden.
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden. AP Photo/Carolyn Kaster

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ametangaza nia yake ya kupendeleza mpango mpya wa mabilioni ya dola mwezi ujao na ameomba kupitishwa haraka kwa mpango unaojadiliwa katika Bunge la Congress baada ya kutangazwa nafasi za ajira zinazokatisha tamaa.

Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa hatutachukua hatua sasa, hatam ya Marekani itakuwa mbaya zaidi. Wamarekani wanahitaji msaada sasa na msaada huo unahitajika mapema mwakani," amesema rais mteule wa Marekani, ambaye atatawazwa kama rais tarehe 20 Januari 2021.

 

Wizara ya Kazi ya Marekani imeripoti kuwepo na nafasi 245,000 za ajira mwezi uliopita, ikiwa ni nafasi ndogo kabisa tangu mwezi Mei.

 

Mpango unaojadiliwa sasa katika Bunge la Congress kushughulikia mgogoro wa afya unaosababishwa na Corona, ambao unakadiriwa kuwa dola bilioni 908, "ni muhimu lakini ni mwanzo tu. Bunge litalazimika kuchukua hatua tena mnamo mwezi Januari" , ameongeza Joe Biden, akizungumza na waandishi wa habari huko Wilmington.

 

"Tunafikiria mamia ya mabilioni ya dola. Nadhani watu watanufaika zaidi na mpango huo," amebaini Joe Biden.