MAREKANI-CHINA

Marekani kuichukulia China vikwazo vipya

Marekani  inajiandaa kuchukuwa vikwazo dhidi ya maafisa kadhaa wa China juu ya jukumu lao kwa kuwatimua wabunge kadhaa wa  huko Hong Kong, kulingana na vyanzo vitatu vilivyonukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Marekani kuiwekea China vikwazo vipya
Marekani kuiwekea China vikwazo vipya AFP/FRED DUFOUR
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo, ambayo inaweza kuchukuliwa kuanzia leo Jumatatu, itawalenga maafisa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CCP).

Utawala wa Donald Trump uunaendelea kuchukuwa vikwazo dhidi ya China Beijing katika wiki za mwisho za mamlaka yake.

Wizara ya mambo ya Nje na na Ikulu ya White House hawakutoa maelezo zaidi kuhusiana na hatua hiyo.

Watu 14, ikiwa ni pamoja na maafisa wa bunge la China au Bunge la kitaifa la Watu China, na maafisa wa chama cha CCP, watalengwa na hatua hiyo kwa kuzuiliwa mali zao na vikwazo vya kifedha, kulingana na vyanzo viwili vilivyonukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Afisa wa Marekani, ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameliambia shirika la habari la REUTERS kwamba watu kadhaa watakabiliwa na vikwazo hivyo vya Marekani.

Vyanzo hivyo havikutaja majina yao au nafasi wanazoshikilia serikalini.