VENEZUELA-SIASA-MADURO

Venezuela: Upinzani wazindua mashauriano ya kiraia kupinga uchaguzi wa wabunge

Rais wa Venezuela  Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro REUTERS/Manaure Quintero

Baada ya matokeo ya uchaguzi wa wabunge kutangazwa nchini Venezuela, sehemu kubwa ya wapinzani waliosusia uchaguzi huo imeanzisha mashauriano ya kiraia. Tangu Jumatatu hadi Jumamosi, wananchi wa Venezuela waliombwa kususia uchaguzi huo wa wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumatatu, wapiga kura walitakiwa kupiga kura kupitia programu ya kupakua kwenye simu ya mkononi na pia kupitia wavuti, au mpiga kura mwenyewe kupiga kura siku ya Jumamosi katika vituo vya kupigia kura ambavyo viliwekwa katika maeneo mbalimbali nchini Venezuela na nje ya nchi, katika nchi ambazo kunaripotiwa idadi kubwa ya raia wa Venezuela.

Kwa upande wa Maria Lopez, anasema kila mtu anahitaji kushiriki na kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guaido, "ili ajue kwamba sisi sote tunahitaji mabadiliko nchini."

Lengo pia ni kuhamasisha wafuasi wa upinzani. Wito huu pia umeelekezwa kwa jamii ya kimataifa, ambayo imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa wabunge, lakini uungwaji wao mkono kwa Juan Guaido ni mdogo ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita. Hali inayomtiwa wasiwasi Ana Rosario Contreras, mwenyekiti wa chama cha Wauguzi jijini Caracas.

"Huu ndio utaratibu Wavenezuela wataamua katika mashauriano haya. Kuweka wazi haja ya kupata usaidizi wa kimataifa ili siku moja nchi hii iweze kuandaa uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika.

Tunahitaji nchi hizi 60, ambazo zilikuwa zikishirikiana kwa kumuunga mkono Juan Guaido, ziunge mkono Venezuela. Na naomba msaada kutoka kwa wananchi wa Ufaransa, kutoka kwa serikali ya Ufaransa, msaada wenu ni muhimu, " amesema Rosario Contreras.

Siku ya Jumatatu wiki hii Tume ya Uchaguzi nchini Venezuela ilitangaza kwamba wagombea wanaomuunga mkono rais Nicolas Maduro wamehakikishiwa kwamba wataendelea kudhibiti bunge kufuatia uchaguzi wa wabunge uliosusiwa na vyama vya upinzani.

Upinzani, ambao ulikuwa na viti vingi katika Bunge lililomaliza muda wake, ulitoa wito wa kususia uchaguzi huo, wakilaani uchaguzi 'usiofaa'.