MAREKANI-CHINA-DIPLOMASIA

Marekani: Biden kumteua Buttigieg kama balozi wa Marekani nchini China

Joe Biden rais mteule wa Marekani
Joe Biden rais mteule wa Marekani AP Photo / Andrew Harnik

Rais mteule wa Marekani Joe Biden anafikiria kumteua meya wa zamani wa mji wa South Bend, katika jimbo la Indiana na mpinzani wa zamani katika kura za mchujo katika chama cha Demokratic, Pete Buttigieg, kuwa balozi nchini China, kulinganan na gazeti la Axios.

Matangazo ya kibiashara

Pete Buttigieg, mwanajeshi wa zamani aliyepigana nchini Afghanistan, alikuwa miongoni mwa wagombea wakuu kwenye nafasi ya balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa lakini, kulingana na Gazeti la Axios, Joe Biden amechagua kutompa jukumu hili.

Hakuna taarifa zaidi ziliyotolewa mara moja na huduma za rais mteule wa Marekani.

Wengi katika safu ya Chama cha Democratic wanaamini kuwa Pete Buttigieg bado ni "anachunguzwa", Gazeti la Axios limeandika, huku likiongeza kuwa kumteua kama balozi wa Marekani nchini China kunaweza kuipatia Beijing matumaini kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na rais huyo mteule wa Marekani.

Tovuti ya hii ya habari inaongeza, hata hivyo, kwamba jina la Pete Buttigieg pia linatajwa kwenye nafasi za juu nchini Marekani.

Pete Buttigieg alikua mmoja wa wasemaji wakuu wa Joe Biden wakati wa kampeni ya uchaguzi dhidi ya rais kutoka chama cha Republican aliyeko madarakani Donald Trump baada ya kupoteza nafasi katika kura za mchujo za chama cha Democratic.