MAREKANI-AFYA-COVID 19

Coronavirus: Zaidi ya vifo vipya 3,200 vyathibitishwa nchini Marekani, rekodi ya kila siku

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump MANDEL NGAN / AFP

Marekani kwa mara ya kwanza imepitisha idadi ya vifo 3,000 kutokana na janga la Corona kwa siku moja tu siku ya Jumatano, wakati maafisa wa afya wameongeza maandalizi ya kutolewa kwa chanjo, kwa kusubiri idhini kutoka Mamlaka ya Dawa ya Shirikisho.

Matangazo ya kibiashara

COVID-19 ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 3,253 nchini Marekani kwa moja tu ya siku ya Jumatano, kulingana na takwimu rasmi, na kufanya idadi ya vifo kufikia 289,740 tangu kuuka kwa mgogoro wa kiafya nchini Marekani.

Visa vipya 220,900 vya maambukizi pia vimerekodiwa, kwa jumla ya watu zaidi ya milioni 15.38 walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani.

Idadi ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini kote nchini ilikuwa 106,217 Jumatano jioni, ikiwa ni rekodi nyingine tangu kuzuka kwa virusi hivyo nchini humo, ikiwa ni sawa na ongezeko la 18% katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Maafisa wa afya wameonya kuwa janga hilo linaweza kuwa mbaya wakati wa msimu wa baridi na wakati huu Marekani ikijiandalia sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.