MAREKANI-SIASA-BIDEN

Marekani: Mtoto wa Joe Biden akabiliwa na uchunguzi katika masuala ya kodi

Hunter Biden, mtoto wa rais mteule wa Marekani  Joe Biden.
Hunter Biden, mtoto wa rais mteule wa Marekani Joe Biden. AP Photo/Pablo Martinez Monsivais

Hunter Biden, mtoto wa rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema katika taarifa kwamba analengwa na uchunguzi katika jimbo la Delaware kuhusu hali yake ya kodi.

Matangazo ya kibiashara

Hii ndio hatua dhaifu ya Joe Biden, yule ambaye Donald Trump alijaribu kumtumia wakati wote wa kampeni, akiita familia ya Biden 'kundi la wahalifu.'

Uchunguzi juu ya mtoto wake Hunter ulizinduliwa mnamo mwaka wa 2018 lakini ulibaki kuwa siri ili kuepuka kushawishi uchaguzi. Uchaguzi sasa umekwisha na Jumanne hii, Desemba 8, wachunguzi waliomba kumsikiliza mtoto wa rais mteule, Hunter Biden.

Hunter Biden, mwenye umri wa miaka 50, inaaminika alishindwa kutangaza mapato yake yote kuhusiana na shughuli zake za kifedha nchini China.

"Nilipata taarifa siku ya Jumatatu kwamba mwendesha mashitaka wa mji wa Delaware anachunguza maswala yangu ya kodi," mtoto wa rais mteule alitangaza katika taarifa Jumatano wiki hii.

"Ninachukulia jambo hili kwa umakini sana," alisema, "na nina hakika kuwa uchunguzi wa kina na wa kweli utaonyesha kuwa niliendesha mambo yangu kisheria. "

"Rais mteule Biden anamuamini sana mwanawe, ambaye amelazimika kukabiliana na changamoto mbaya, ikiwa ni pamoja na mashambulio mabaya ya kibinafsi katika miezi ya hivi karibuni, ili hatimaye aweze kushinda na kuwa imara," timu ya mpito ya Joe Biden imesema katika taarifa hiyo.

Jaribio la kwanza kwa rais mteule

Akikabiliwa na Donald Trump katika mjadala wa mwisho wa televisheni, Joe Biden alikanusha kuhusika kwa kwa kesi hizi, lakini hiyo haizuii Warepublican kulalamika juu ya mzozo wa kimaslahi.

Donald Trump anamshtumu Hunter Biden kuwa alinufaika kifedha kwa kiasi kikubwa kupitia baba yake nchini China na kunufaika zaidi nchini Ukraine, bila hata hivyo kulipa kodi.

Vyombo vya habari vya Marekani vinaangazi akwa mapana kesi hii na kubaini kwamba ni  jaribio la kwanza kwa rais mteule Joe Biden.